YANGA WATUA KWA MASHINE HII,NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumamosi
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumamosi
PABLO Franco, leo Novemba 26 ameongoza mazoezi kwa mara ya kwanza kwa kikosi chake katika Uwanja wa Mkapa. Mazoezi ya leo ni kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao ni wa mtoano na unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa. Itakuwa ni Novemba 28 ambapo mashabiki 35,000 wa Simba wameruhusiwa kuingia kushuhudia mchezo huo. Kwa…
LIGI Kuu Tanzania kwa sasa ni raundi ya 7 ambapo tayari ratiba ipo wazi na ratiba itakuwa namna hii. Katika ligi vinara ni Yanga wakiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi huku Mtibwa Sugar wakiwa bado hawajafanikiwa kushinda ni wanaburuza mkia.
SIMULIZI ya jamaa aliyekuwa akipapata adhabu kutoka kwa mkewe Ama kwa hakika ndoa huwa rahisi kwa mtu ambaye hajawahi ingia kwenye ndoa. Kwa ufahamu wangu suala zima la ndoa ni ngumu sana haswa ukipata mpenzi asiyekuelewa kwa vyovyote vile ama aliye na kazi nzuri kuliko wewe kama mume. Mapenzi huwa na mambo mbalimbali ambayo watu…
WAPINZANI wa Simba katika Kombe la Shirikisho barani Afrika, Klabu ya Red Arrows imeweka wazi kuwa nia yao ya kusonga mbele katika michuano hiyo huku wakitamba kufanya vizuri wakiwa ugenini. Red Arrows kutoka Zambia Jumapili Novemba 28 watacheza mchezo wao wa kwanza wa mtoano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar. Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika Desemba Mosi nchini Zambia ambapo Simba watakuwa ugenini…
RALF Rangnick mwenye umri wa miaka 63 anatarajiwa kupewa majukumu ya kuwa Kocha Mkuu kwa muda ndani ya kikosi cha Manchester United akichukua mikoba ya Ole Gunnar Solskjaer ambaye alichimbishwa ndani ya kikosi hicho. Rangnick atapaswa kuweka kando majukumu yake aliyokuwa akiyafanya ndani ya Lokomotiv Moscow ili kuweza kumpokea kocha wa mpito, Michael Carrick ambaye…
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Ijumaa
MASHABIKI 35,000 ni ruksa kuushuhudia mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Novemba 28. Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika, (CAF) ni mashabiki hao wataruhusiwa kuwa ndani ya uwanja kushuhudia mchezo huo. Na pia mashabiki hao wanapaswa kufuata taratibu na kanuni za kujilinda dhidi ya Corona. Unatarajiwa kuwa mchezo mkali…
JESUS Moloko ndani ya Yanga kwa msimu wa 2021/22 amehusika katika mabao mawili kati ya mabao 10 ambayo yamefungwa. Ametupia mabao mawili katika ligi akitumiq pasi ya mshambuliaji wa Yanga, Yacouba Songne raia wa Burkina Faso. Kwa sasa Yacouba yupo nje ya uwanja akipata matibabu zaidi baada ya kupata majeraha alipokuwa akitumikia timu hiyo kwenye…
MBELE ya mastaa wakubwa ambao wanalipwa mkwanja mrefu ikiwa ni pamoja na Lionel Messi, Neymar Jr na Kylian Mbappe bado Manchester City waliibuka wababe. Ni katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Etihad ambao ulikuwa ni wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, City walisepa na pointi tatu mazima. Ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya PSG unaifanya timu hiyo…
KAZI imeanza kwa Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco baada ya kushuhudia namna Ligi Kuu Bara inavyokwenda na kasi ya wachezaji wake ambao alianza nao kikosi cha kwanza. Baada ya kuchukua mikoba ya Didier Gomes kete yake ya kwanza ilikuwa mbele ya Ruvu Shooting, Uwanja wa CCM Kirumba na ubao ulisoma Ruvu Shooting 1-3 Simba.Haya…
MKONGWE wa Manchester United, Paul Scholes ameweka wazi kuwa Michael Carrick hatakiwi kuwa kocha wa moja kwa moja ndani ya kikosi hicho kwa wakati huu kwa kuwa hana uzoefu. Carrick anaiongoza Manchester United kwa muda mara baad ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Ole Gunnar Solkjaer kuchimbishwa kikosini hapo kutokana na mwendo mbovu wa tim…
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Alhamisi
MWANDISHI nguli kwenye sekta ya michezo wa magazeti ya Championi na Spoti Xtra, Saleh Ally, ‘Jembe’ amechaguliwa na Shirikisho la Kimataifa, (Fifa) kuwa mwandishi pekee kutoka Tanzania kupiga Kura kwenye Tuzo za Mchezaji Bora wa Fifa zinazotarajiwa kufanyika Januari 17,mwakani.
KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameweka wazi kuwa wao kama wachezaji wanaendelea kujipanga kuhakikisha wanapata alama tatu kwenye michezo yao inayofuata kwani msimu huu wana jambo lao hivyo mashabiki wasiwe na wasiwasi. Yanga hadi sasa inaongoza Ligi Kuu Bara kwa pointi 16 katika michezo yote sita iliyocheza hadi sasa huku ikifuatiwa na Simba wenye pointi 14. Feisal alisema kuwa kama safari ndio kwanza imeanza ya kusaka ubingwa, hivyo wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata alama tatu kwenye mechi zao…
WASHINDI wamezidi kupewa mkwanja kutoka Sportpesa Jacpot bonus baada ya kuweza kushinda. Yote hii inatokana na kuweza kubashiri kwa usahihi mechi ambazo zinaendelea kwa sasa. Pichani ni mshindi wa Sportpesa Jackpot bonus Aichat Haroun Abdallah(23) kutoka Kigamboni, DSM akishikilia mfano wa hundi ya shilingi 6,753,390 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 11 kati ya 13 kwenye…
UONGOZI wa Klabu ya DTB inayoshiriki Championship umeeleza kuwa mchezo wao uliotarajiwa kuchezwa Novemba 28 sasa umesogezwa mbele itakuwa ni Novemba 29. Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa DTB, Juma Ayo amesema kuwa mchezo huo umepelekwa mbele kupisha mchezo wa kimataifa kati ya Simba dhidi ya Red Arrows utakaochezwa Uwanja wa Mkapa ambao ni…