>

KOCHA MANCHESTER UNITED UZOEFU TATIZO

MKONGWE wa Manchester United, Paul Scholes ameweka wazi kuwa Michael Carrick hatakiwi kuwa kocha wa moja kwa moja ndani ya kikosi hicho kwa wakati huu kwa kuwa hana uzoefu.

Carrick anaiongoza Manchester United kwa muda mara baad ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Ole Gunnar Solkjaer kuchimbishwa kikosini hapo kutokana na mwendo mbovu wa tim hiyo katika Ligi Kuu England.

Mrithi huyo wa mikoba ya Ole kwa muda ameiongoza timu hiyo kwenye mchezo mmoja iliku dhidi ya Villarreal ambao ni wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na aliweza kushinda na kuipelekea timu hiyo hatua ya 16 bora.

Mkongwe huyo ameweka wazi kuwa hafikirii kama Michael anaweza kupewa timu kwa kuwa anajua Manchester United watatafuta kocha mwingine kwani kocha huyo hana uzoefu.

“Sidhani kama anaweza kuongoza,ila sijui nani anajua hilo. Baada ya mechi ya Chelsea kuna mechi 10 ambazo anaweza kushinda.Lakini hii ni Manchester United inatakiwa kuongozwa na kocha bora.

“Michael Carrick? Kocha mkuu wakati kasimamia mechi moja hapana. Hana uzoefu ndiyo ukweli huwezi kumpatia timu anahitajika kocha mwenye uzoefu na bora na bora wa kuiongoza timu,”.