
HAYA HAPA MATOKEO YA RAUNDI YA 30, MWISHO WA RELI KIGOMA KUGUMU
MZUNGUKO wa 30 umegota mwisho huku yakikusanywa mabao 26 uwanjani ni Uwanja wa Lake Tanganyika…
MZUNGUKO wa 30 umegota mwisho huku yakikusanywa mabao 26 uwanjani ni Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma pekee ngoma ilikuwa ngumu kwa wababe hao kushuhudia bao kwa upande wowote ule ikiwa ni funga kazi ndani ya msimu wa 2024/25. Katika raundi ya 29 ni mabao 22 yalifungwa hivyo kasi imeongezeka raundi ya 30 yakiongezeka mabao manne…
Klabu ya Yanga SC imeonyesha ubabe wake kwa kuichapa Dodoma Jiji mabao 5-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa kwenye Dimba la New Amaan Complex, visiwani Zanzibar. Kwa ushindi huo mnono, Yanga si tu imejiongezea morali, bali pia imetuma ujumbe mzito kwa Simba kuwa wako tayari kwa vita ya kukata ubingwa au kulinda…
Ni rasmi sasa! Kagera Sugar imeshuka daraja kutoka Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Simba SC kwenye mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Kagera Sugar, moja ya timu zenye historia ya muda mrefu katika ligi hiyo, sasa inajiandaa kwa maisha ya Championship msimu ujao.
MKALI anayekimbiza kunako Bongo Fleva, Mbwana Yusuf Kilungi almaarufu kama Mbosso Khan, ametikisa tena anga ya muziki kupitia ngoma yake mpya “Aviola (Bonge la Dada).” Wimbo huu ambao tayari unafanya vizuri mitandaoni na kwenye vituo vya redio, umekuwa kivutio kikubwa kwa wapenzi wa burudani kutokana na mdundo wake wa kuvutia, mashairi yenye hisia kali, pamoja…
Mchezo wa Fountain Gate vs Azam FC, Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa Juni 22 2025 patachimbika uwanjani kwa wababe hao kuvuja jasho kusaka ushindi ndani ya dakika 90. Fountain Gate hesabu kubwa ni kujinasua kutoka mstari wa kucheza play off huku Azam FC hesabu kubwa ikiwa ni kumaliza ndani ya tatu bora ikiwa na pointi nyingi….
Usiku wa kuamkia Juni 22, 2025, jiji la Dar es Salaam liligeuka kuwa kitovu cha burudani baada ya kufanyika kwa uzinduzi wa Heineken Silver kinywaji kipya kilichokuja na ladha laini lakini kisicho na mpinzani. Uzinduzi huo umefanyika Mlimani City na uliandaliwa kwa ubunifu wa hali ya juu, na kuonyesha kiwango kipya cha hafla zenye hadhi…
Kampuni inayoaminika zaidi kwenye michezo ya kubashiri nchini Tanzania, Meridianbet, imeleta tena promosheni inayotikisa. Mwezi huu wa Juni, usikose kushiriki katika ofa kabambe iitwayo “Paa na Super Heli, Shinda Samsung A25”, promosheni maalum kwa wachezaji wa kasino mtandaoni, hasa mchezo wa Super Heli. Kupitia promosheni hii, unapata nafasi ya kushinda simu mpya aina ya Samsung…
BAADA ya kucheza mechi 28 ambazo ni dakika 2,520 safu ya ushambuliaji ya Yanga SC imefunga mabao 76 na kukusanya pointi 76 ikiwa namba moja kwenye msimamo na timu iliyofunga mabao mengi. Kwenye mchezo wake wa raundi ya 29 dhidi ya Tanzania Prisons, Yanga SC ilikomba pointi tatu mazima kwa ushindi wa jumla ya mabao…
Kwenye eneo la tuzo ya kiatu cha ufungaji bora vita bado ni mbichi kutokana na mechi ambazo zimebaki matokeo yake kutotabirika. Jean Ahoua wa Simba SC ni kinara kwa sasa akiwa na mabao 16 anafuatiwa na Clement Mzize na Prince Dube wa Yanga SC wakiwa wametupia mabao 13. Leonel Ateba wa Simba SC naye katupia…
Meridianbet leo hii imekuja na promo kabambe kabisa ya 3 OAKS ambayo imetua jana hivyo mteja wa Meridianbet una siku 13 tuu za kuwania pesa taslimu mpaka milioni moja. Nafasi ni yako leo furahia ushindi mnono hapa. Jana tarehe 20 ndio mashindano haya ya 3 OAKS na yatamalizika 3 Julai mwaka 2025 ambapo wateja…
Yanga SC msimu wa 2024/25 wamevunja rekodi ya mabao yakufunga katika mechi za Ligi Kuu Bara ambayo waliiandika msimu wa 2023/24. Yanga SC ilifunga mabao 71 baada ya mechi 30 na ilitwaa ubingwa wa ligi hivyo ni mabingwa watetezi. Msimu wa 2024/25 baada ya mechi 28, Yanga SC imefunga jumla ya mabao 76 ongezeko la…
LIGI Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora inatarajiwa kugota mwisho Juni 22 kwa mechi za raundi ya 30 kupigwa kwenye viwanja 8 tofautitofauti. Mechi zote 8 zitaonyeshwa mubashara Azam TV kuanzia saa 10:00 ambapo mechi zote zonatarajiwa kuonyeshwa na JKT Tanzania watakuwa kwenye Sinema Zetu. Hii hapa ratiba ya Juni 22 2025…
YANGA SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi kwa msimu wa 2024/25 imempiga jumla ya mabao 9-0 mpinzani wake Tanzania Prisons kwenye mechi mbili za ligi katika msako wa pointi tatu. Yanga SC imekomba pointi sita mazima ikijikita kileleni ndani ya ligi ambayo inakaribia kugota mwisho Juni 25 2025. Juni 18 2025 kwenye mchezo wa…
Kampuni kubwa ya ubashiri Tanzania, Meridianbet leo hii iliamua kufunga safari moja kwa moja mpaka mtaa wa Mpakni Kinondoni B na kugawa mapipa ya taka kwa lengo la kuwezesha ukusanyaji mzuri wa taka na kudumisha mazingira safi. Katika tukio hilo la kutoa mapipa hayo ya taka, Meridianbet ilisema kuwa vifaa hivyo vina lengo la…
Meridianbet inazidi kuwapa wateja wake nafasi za kipekee kushinda zaidi kupitia chaguo lae la GG&3+ na utapata mara mbili zaidi. Katika mechi kali ya Inter Miami vs FC Porto, bashiri ya GG & 3+ ndiyo tiketi yako ya ushindi maradufu. Bashiri kuwa timu zote zitafunga (GG) na kutakuwa na zaidi ya magoli matatu (3+) na…
Heineken Silver made a bold and unforgettable debut in Tanzania, launching not just a drink, but a revolution in nightlife. Held underground for the first time ever, the launch event broke tradition and redefined premium experiences for a new generation. In a move that set a new standard, the event had no VIP section; every…
Baada ya dakika 90 kukamilika mzunguko wa 29 jumla yamefungwa mabao 22 kutoka katika viwanja 8 tofautitofauti msimu wa 2024/25 kwenye msako wa pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90. Kutoka viwanja 8 ni Uwanja wa Majaliwa pekee dakika 90 ziligota mwisho bila kupatikana kwa bao kwa timu zote mbili ambapo ubao ulisoma Namungo FC…