KIGAMBONI NA MERIDIANBET NI DAMUDAMU

Meridianbet na Kigamboni ni damudamu kwani wamekua na ushirikiano mzuri katika matukio mbalimbali, Ndio sababu Meridianbet wamefika tena Mei 25, 2024 eneo hilo na kuigusa jamii ya watu wa Kigamboni.

Mabingwa hao wa michezo ya kubashiri walifika Kigamboni kwenye eneo la Mji mwema kutoa msaada wa Reflectors kwa Bodaboda wanaopatikana katika eneo hilo, Lakini pia walifanikiwa kufika Zahanati ya eneo hilo na kutoa vifaa vya usafi.

Meridianbet wamekua na utaratibu wa kuhakikisha wanarudisha kwenye jamii yake pale ambapo wanapata nafasi ya kufanya hivo, Kwani wanaamini jamii inakumbwa na matatizo mengi ambayo yanahitaji utatuzi.

Lengo kubwa la kutoa msaada haswa kwenye Zahanati wa vifaa vya usafi ni kuhakikisha wanaimarisha usafi katika eneo hilo, Kwani eneo ambalo linatoa huduma za kiafya ni eneo muhimu zaidi na linapaswa kua na mazingira safi.

Msaidizi wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko kutoka Meridianbet bwana Abubakar Kulindwa alipata nafasi ya kuzungumza machache baada ya kukabidhi vifaa ambapo alisema “Nina furaha kubwa kufika eneo hili na mapokezi ambayo nimeyapata lakini kubwa zaidi ni sisi kuguswa na jamii ambayo imetuzunguka na kuhakikisha tunajaribu kupunguza baadhi ya matatizo ambayo yanaikabili na tunamshukuru Mungu tumelifanikisha hilo kwa ushirikiano wenu mkubwa”.

Suka mkeka wako kwenye michezo mikali ya itakayopigwa katika ligi mbalimbali barani ulaya wikiendi hiiMachaguo zaidi za 1000 yapo huku lakini vile vile Turbo Cash pia ipo. Unasubiri nini sasa? Ingia meridianbet na ubashiri sasa.`

Aidha Mganga wa eneo hilo aliweza kufurahishwa na kitendo hicho kilichofanywa na mabingwa hao wa michezo ya kubashiri nchini Tanzania, Huku akitoa wito kwa makampuni mengine kuweza kufata nyayo za Meridianbet katika kuhakikisha wanaikumbuka jamii yao.