FT:MECHI MZUNGUKO WA PILI, AZIZ, FEI NGOMA NZITO

MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu Bara mechi nane zimechezwa na kurushwa mubashara Azam TV huku nyota wawili Feisal Salum wa Azam FC na Aziz KI wa Yanga kila mmoja akifunga kwenye mchezo husika.

Fei kafunga mabao mawili dhidi ya Kagera Sugar akifikisha mabao 18 sawa na Aziz KI ambaye amefunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Tabora United ambapo Yanga imeshinda mabao 3-0.

Haya hapa matokeo ya mechi hizo dakika 45 za mwanzo namna hii pamoja na sehemu inayorushwa na Azam TV:-

Simba 1-0 KMC.

Azam 5-1 Kagera Sugar.

Singida 2-1 Geita Gold.

Namungo 2-2 TZ Prisons.

Ihefu 0-2 Dodoma Jiji.

Mashujaa 3-2 Mtibwa Sugar.

Coastal Union 0-0 JKT Tanzania.

Yanga 3-0 Tabora United.