YANGA 1-0 TAIFA JANG’OMBE, DAKIKA 45

MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi Yanga wanakwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao moja kwa nunge.

Dakika 45 zimekamilika na ubao unasoma Yanga 1-0 Taifa Jang’ombe.

Bao la kuongoza limefungwa na Heritier Makambo dakika ya ya 32 akiwa nje ya 18.

Pia nyota mpya wa Yanga Dennis Nkane ameanza kikosi cha kwanza leo Januari 5,2022 na ameweza kuonyesha makeke yake.