LEONEL ATEBA AFIKISHA MATANO SIMBA IKISHINDA MBELE YA KEN GOLD

MSHAMBULIAJI wa Simba, Leonel Ateba Desemba 18 2024 amefunga mabao mawili yaliyoipa pointi tatu muhimu timu hiyo kwenye mchezo dhidi ya Ken Gold.

Ni dakika ya 34 Ateba alipachika bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti iliyosababishwa na Awesu Awesu na dakika ya 44 alipachika bao la pili kwa pigo la kichwa akimalizia kona iliyopigwa na Nouma.

Kipindi cha kwanza mabao yote mawili yalifungwa huku beki Che Malone dakika ya 78 pasi yake aliyopoteza iliongeza hatari kwenye eneo la Simba kutokana na Ken Gold kufanya shambulizi ambalo halikuwa na faida kwao.

Joshua Mutale alianzia benchi na aliingia kipindi cha pili kama ilivyokuwa kwa Jean Ahoua ambaye dakika ya 90 alitengeneza jaribio lililomshinda Ateba kulitumia kwa umakini akiwa ndani ya 18.

Simba inafikisha pointi 31 ndani ya ligi huku Ken Gold ikisalia na pointi zake sita baada ya kucheza mechi 15.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.