>

SIMBA YASHINDA MABAO 2-0 SELEM VIEW,KOMBE LA MAPINDUZI

SELEMAN Matola kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa ushindi ambao wameupata leo ni furaha kwao na pongezi kwa wachezaji.

Ushindi wa mabao 2-0 dhidi Selem View ambao walikwama kupiga shuti ambalo limelenga lango mbele ya Simba.

Ni mabao ya Pape Sakho dakika ya 24 na liliweza kudumu mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Simba walipachika bao dakika ya 53 na kuwafanya Simba kuondoka na ushindi katika kundi C na wanakibarua cha kusaka ushindi katika mchezo wao ujao dhidi ya Mlandege.

“Furaha kwetu kupata pointi tatu na pongezi kwa wachezaji namna ambavyo wameweza kufanya hivyo kazi bado inaendelea,”.

Kwenye mchezo wa leo Rally Bwalya amechaguliwa kuwa mchezaji bora na amesepa na zawadi ya shilingi laki tano.