>

DAKIKA 45,SIMBA 1-0 SELEM VIEW, KOMBE LA MAPINDUZI

UWANJA wa Amaan kwa sasa ni mapumziko mchezo wa Kombe la Mapinduzi na timu zote zimeyeyusha dakika 45.

Ubao unasoma Simba 1-0 Selem View na mashabiki wengi wamejitokeza kushuhudia mchezo huu.

Ni bao la Pape Sakho aliyepachika bao hilo dakika ya 24 na kuifanya Simba kuwa mbele kwa bao hilo.

Leo langoni kwa Simba ni kipa Beno Kakolanya ambaye mwaka 2021 aliweza kukaa langoni pia na Simba ilitinga hatua ya fainali na kupoteza kwa kufungwa penalti.