NYOTA Gerald Mdamu aliyewahi kukipiga ndani ya Polisi Tanzania bado anapambania hali yake ili kurejea kwenye ubora wake mdogomdogo baada ya kuumia mguu walipopata ajali ya gari wakitokea mazoezini.
Julai 9 2021 ilikuwa ni ganzi ya maumivu kwenye ulimwengu wa mpira baada ya ajali hiyo kutokea na mchezaji aliyeumia zaidi kuliko wote alikuwa ni Mdamu.
Akizungumza na Spoti Xtra Regan Senya mtu wa karibu wa Mdamu alisema kuwa mchezaji huyo anahitaji msaada kwa kuwa ana mahitaji pamoja na watoto ambao wanasoma huku akiwa bado na ndoto ya kurejea uwanjani.
“Mdamu anaendelea vizuri na taarifa ya awali iliyokuwa inazungumzia kuhusu kupata msaada wa kutoa vyuma ilipokelewa vizuri. Vile vyuma ambavyo vilikuwa vinamsumbua vilitolewa bado vyuma vingine vimebaki.
“Tunahitaji pia kumpata mtaalamu wa mifupa ili afanikishe jambo lake la kurejea uwanjani. Bado ana ndoto za kucheza mpira kwa kuwa ni kitu ambacho anakipenda,”alisema.
Kwa watakaoguswa kumchangia Mdamu namba ni 0655670101 jina Juliana Malekela.
Tottenham Hotspur forward Dominic Solanke battles with Crystal Palace defender Maxence Lacroix during the English championship Premier League football match between Crystal Palace and Tottenham Hotspur on 27 October 2024 at Selhurst Park in London, England - Photo Ian Stephen / ProSportsImages / DPPI (Photo by IAN STEPHEN / ProSportsImages / DPPI via AFP)