HAWA HAPA MAKOCHA WAPYA SIMBA

RASMI uongozi wa Simba umewatambulisha makocha wapya watatu ambao watakuwa na kikosi hicho kutimiza majukumu yao kwenye mechi za kitaifa na kimataifa.

Usiku wa kuamkia Novemba 28 makocha hao wametua Bongo na kupokelewa na viongozi wa Simba wakiongozwa na Mtendaji Mkuu Imani Kajula.

Timu hiyo ilisitisha mkataba wa Roberto Oliveira Novemba 7 muda mfupi baada ya kushuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yanga.

Mchezo huo wa ligi ulichezwa Novemba 5 Uwanja wa Mkapa ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa msimu wa 2023/24 Simba kupoteza.

Ni Kocha mkuu Abdelhak Benchikha, Kocha msaidizi Farid Zemiti na Kocha wa viungo Kamal Boudjenane

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba amesema wanaamini makocha hao watafanya kazi kubwa kuongeza ari ya ushindi kwenye mechi zao zote za ushindani.