Klabu ya Real Madrid imetwaa ubingwa wa kombe la Mabara kufuatia ushindi wa 3-0 dhidi ya Pachuca Fc ya Mexico kwenye fainali iliyopigwa katika dimba la Lusail mjini Lusail, Qatar.
Ushindi wa Real Madrid unamfanya kocha Carlo Ancelotti kuweka rekodi ya kuwa kocha mwenye Mataji mengi zaidi katika historia ya klabu hiyo akifikisha jumla ya makombe 15 na kumpiku Miguel Munoz aliyeinoa klabu hiyo kati ya miaka ya 1960 and 70.
Winga wa Real Madrid Vinicius Jr ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza akitunukiwa mpira wa dhahabu huku Federico Valverde akishinda mpira wa shaba wakati Montiel wa Pachuca akipewa mpira wa Fedha.
FT: Real Madrid 3-0 Pachuca
⚽ 37’ Mbappé
⚽ 53’ Rodrygo
⚽ 84’ Vinicius Jr