Home International KOCHA HUYU HAPA KUIBUKIA MANCHESTER UNITED

KOCHA HUYU HAPA KUIBUKIA MANCHESTER UNITED

RALF Rangnick mwenye umri wa miaka 63 anatarajiwa kupewa majukumu ya kuwa Kocha Mkuu kwa muda ndani ya kikosi cha Manchester United akichukua mikoba ya Ole Gunnar Solskjaer ambaye alichimbishwa ndani ya kikosi hicho.

Rangnick atapaswa kuweka kando majukumu yake aliyokuwa akiyafanya ndani ya Lokomotiv Moscow ili kuweza kumpokea kocha wa mpito, Michael Carrick ambaye anatarajiwa kuiongoza timu hiyo katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Chelsea ambao utakuwa ni wa Ligi Kuu England.

Hatua ambayo ipo kwa sasa inatajwa kuwa imefikia sehemu nzuri kwa kuwa United inafanya mazungumzo na mabosi wa Rangnick ili aweze kujiunga na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.

Pia mbali na kocha huyo pia wengine ambao wanatajwa kuweza kupewa mikoba ya kuwa makocha wa muda ni pamoja na Ernesto Valverde ambaye alikuwa kocha wa zamani wa Barcelona na Kocha wa zamani wa Lyon, Rudi Garcia.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA
Next articleRED ARROWS WAPINZANI WA SIMBA WANA MCHECHETO