Home Sports SIMBA V RED ARROWS YAPELEKA MBELE RATIBA CHAMPIONSHIP

SIMBA V RED ARROWS YAPELEKA MBELE RATIBA CHAMPIONSHIP

 

UONGOZI wa Klabu ya DTB inayoshiriki Championship umeeleza kuwa mchezo wao uliotarajiwa kuchezwa Novemba 28 sasa umesogezwa mbele itakuwa ni Novemba 29.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa DTB, Juma Ayo amesema kuwa mchezo huo umepelekwa mbele kupisha mchezo wa kimataifa kati ya Simba dhidi ya Red Arrows utakaochezwa Uwanja wa Mkapa ambao ni wa Kombe la Shirikisho.

“Mhezo wetu dhidi ya Ndanda FC uliopangwa kuchezwa Novemba 28 umepelekwa mbele mpaka Novemba 29 Uwanja wa Uhuru.

“Sababu za kusogezwa mbele ni kupisha mchezo wa kimataifa kati ya Simba na Red Arrows utakaochezwa Novemba 28,Uwanja wa Mkapa.

” Mashabiki wa DTB tunaomba radhi kwa mabadiliko haya,tujitokeze kwa wingi siku husika kwa ajili ya kuishangilia timu yetu,” amesema.

DTB ni namba moja kwenye ligi wakiwa na jumla ya pointi 18 baada ya kucheza mechi 8 msimu huu wa 2021/22.

Previous articleWAAMUZI NI PASUA KICHWA,WACHEZAJI PIGENI KAZI
Next articleAICHAT ASHINDA JACKPOT YA SPORTPESA MKWANJA WAKE NOMA