>

MOLOKO NDANI YA YANGA AHUSIKA KATIKA MABAO MAWILI

JESUS Moloko ndani ya Yanga kwa msimu wa 2021/22 amehusika katika mabao mawili kati ya mabao 10 ambayo yamefungwa.

Ametupia mabao mawili katika ligi akitumiq pasi ya mshambuliaji wa Yanga, Yacouba Songne raia wa Burkina Faso.

Kwa sasa Yacouba yupo nje ya uwanja akipata matibabu zaidi baada ya kupata majeraha alipokuwa akitumikia timu hiyo kwenye mchezo wa ligi.

Katika msimamo Yanga ipo nafasi ya kwanza na pointi zake ni 16, baada ya kucheza mechi 6 imeshinda mechi tano na sare moja.

Sare yake ya kwanza msimu wa 2021/22 ilikiwa mbele ya Namungo FC mchezo dume uliochezwa Uwanja wa Ilulu,Lindi.