>

MASHABIKI RUKSA MECHI YA SIMBA V RED ARROWS KWA MKAPA

MASHABIKI 35,000 ni ruksa kuushuhudia mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Novemba 28.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika, (CAF) ni mashabiki hao wataruhusiwa kuwa ndani ya uwanja kushuhudia mchezo huo.

Na pia mashabiki hao wanapaswa kufuata taratibu na kanuni za kujilinda dhidi ya Corona.

Unatarajiwa kuwa mchezo mkali na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi.

Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco itakuwa ni kibarua chake cha kwanza katika mechi za kimataifa baada ya kurithi mikoba ya Didier Gomes.

Mchezo wa kwanza kukaa benchi ilikuwa dhidi ya Ruvu Shooting na alishinda mabao 3-1 ila ulikuwa ni wa Ligi Kuu Tanzania Bara.