MBELE ya mastaa wakubwa ambao wanalipwa mkwanja mrefu ikiwa ni pamoja na Lionel Messi, Neymar Jr na Kylian Mbappe bado Manchester City waliibuka wababe.
Ni katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Etihad ambao ulikuwa ni wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, City walisepa na pointi tatu mazima.
Ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya PSG unaifanya timu hiyo kutinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Inafikisha jumla ya pointi 12 ikiwa nafasi ya kwanza na PSG ipo nafasi ya pili na pointi zake ni 8 zote zimecheza mechi tano.