>

FEI TOTO ASHUSHA PRESHA YANGA

KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameweka wazi kuwa wao kama wachezaji wanaendelea kujipanga kuhakikisha wanapata alama tatu kwenye michezo yao inayofuata kwani msimu huu wana jambo lao hivyo mashabiki wasiwe na wasiwasi.


Yanga hadi sasa 
inaongoza Ligi Kuu Bara kwa pointi 16 katika michezo yote sita iliyocheza hadi sasa huku ikifuatiwa na Simba wenye pointi 14.


 Feisal alisema kuwa kama safari ndio kwanza imeanza ya kusaka ubingwa, hivyo wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata alama tatu kwenye mechi zao zinazofuata.

 

“Tunamshukuru Mungu hadi hapa tulipofikia tunaongoza ligi lakini hiyo pekee haitoshi kutufanya turidhike, hivyo tunaendelea kupambania malengo ya timu kwa sababu sisi wachezaji ndio tuna dhamana kubwa ya kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri kwa kupambana uwanjani.


“Kwa hiyo kitu pekee 
ninachoweza kuwaambia mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi kwani tumejipanga vizuri sana msimu huu tuna jambo letu kubwa ambalo kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu litatimia,” alisema mchezaji huyo.

 

Chanzo:Championi