Home Sports SIMBA YAIPIGIA MATIZI RED ARROWS KWA MKAPA

SIMBA YAIPIGIA MATIZI RED ARROWS KWA MKAPA

PABLO Franco, leo Novemba 26 ameongoza mazoezi kwa mara ya kwanza kwa kikosi chake katika Uwanja wa Mkapa.

Mazoezi ya leo ni kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao ni wa mtoano na unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Itakuwa ni Novemba 28 ambapo mashabiki 35,000 wa Simba wameruhusiwa kuingia kushuhudia mchezo huo.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wanaimani yakuweza kupata ushindi.

‘Tunajua mchezo utakuwa mgumu na mwalimu ameweka wazi kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo mashabiki wajitokeze kwa wingi,”.

Previous articleRATIBA YA LIGI KUU BARA MZUNGUKO WA 7
Next articleYANGA WATUA KWA MASHINE HII,NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI