
BANGALA AANDALIWA KWA AJILI YA SIMBA
YANGA imedhamiria kuwafunga kwa mara pili watani wao Simba, ni baada ya kumpumzisha kwa makusudi kiungo wao mkabaji, Mkongomani Yannick Bangala katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara. Mchezo ujao wa ligi wa Yanga watacheza dhidi ya Mbeya Kwanza kwenye Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya ambao Bangala atakuwepo jukwaani akiutazama mchezo huo. Dabi hiyo inatarajiwa kupigwa Desemba 11, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam katika mchezo uliopita wa Ngao ya Jamii uliozikutanisha timu hizo, Yanga ilifanikiwa kuwafunga Simba bao 1-0…