Home Sports MABOSI SIMBA WAMUWEKEA MTEGO PABLO

MABOSI SIMBA WAMUWEKEA MTEGO PABLO

WAKATI kesho Pablo Franco akiwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Red Arrows katika mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho, mabosi wa Simba wamempa mtego kocha wao kwa kumpa malengo makubwa ambayo anapaswa kuyafikia.
Pablo amerithi mikoba ya Didier Gomes ambaye aliomba kuondoka baada ya timu hiyo kuboronga katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ilifungwa mabao 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy, Uwanja wa Mkapa.
Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa wamezungumza na Pablo ili kuweza kufaya vizuri kimataifa.
“Mpango wetu wa kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika haukutimia kwa bahati ila tunashukuru Mungu timu ipo katika Kombe la Shirikisho na haya pia ni mashindano ya kimataifa.
“Ambacho tumemwambia Pablo ni kwamba tunahitaji kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho inawezekana kwani wachezaji wapo tayari na kila kitu kipo sawa,” amesema Barbara.
Kwenye mchezo huo wa kesho ambao ni wa mtoano tayari wapinzani wa Simba wamewasili Tanzania ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya mwisho.
Jana,Novemba 26 Simba walifanya mazoezi Uwanja wa Mkapa kwa ajili ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Previous articleTENGENEZA MKWANJA KWENYE MICHEZO YA KIBABE WIKIENDI HII
Next articleSTERLING KUSAINI DILI JIPYA CITY