Home International RONALDINHO ANUKIA JELA ISHU YA MAPENZI

RONALDINHO ANUKIA JELA ISHU YA MAPENZI

NYOTA wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na Klabu ya Barcelona na AC Milan, Ronaldinho ameonywa kwamba anaweza kuibukia jela ikiwa atashindwa kumlipa mgawo wa mali mpenzi wake wa zamani ifikapo Desemba Mosi mwaka huu.

Taarifa kutoka nchini Brazil zimeeleza kuwa nyota huyo mwenye miaka 41 ametakiwa kumaliza ishu hiyo na Priscilla Coelho ifikapo Desemba Mosi ili kuepusha mali zake kuzuiwa na ikiwezekana kwenda jela.

Mwanasheria wa Priscilla, Bruno Medrado ameliambia Gazeti la Extra la nchini Brazil kuwa hakuna ujanja mwingine ambao unaweza kufanyika..

“Kwa sasa hana ujanja anapaswa kulipa tu,” hata hivyo haijatajwa ni kiasi gani nyota huyo anapaswa kulipa.

Mei 2018,Ronaldinho alikanusha kuwa alikuwa amemuoa mrembo huyo na mwanamke mwingine kwa mpigo, aliyetajwa kwa jina la Beatriz Sousa.

Previous articleSTERLING KUSAINI DILI JIPYA CITY
Next articleSIMULIZI YA ALIYEACHWA KISA MKWANJA