
KISA KUVULIWA UBINGWA,MWAKINYO ASEMA NI WIVU TU
BAADA ya Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBF), kuwavua mikanda yao ya ubingwa wa Intercontinetal, Hassan Mwakinyo na Ibrahim Class, hatimaye bondia Hassan Mwakinyo ameibuka na kuvunja ukimya kwa kusema kuwa yeye na uongozi wake haujui chochote zaidi ya kudai kuonewa wivu. Mwakinyo ametoa kauli hiyo kufuatia WBF kuwavua mkanda ya ubingwa huo, kwa kuzingatia kanuni inayotamka kuwa bondia akishindwa kutetea ubingwa wake ndani ya miezi sita tangu aupate, basi atavuliwa. Rais wa…