Home Sports PABLO:TUTACHEZA KWENYE UWANJA AMBAO TUNAWEZA KUCHEZA

PABLO:TUTACHEZA KWENYE UWANJA AMBAO TUNAWEZA KUCHEZA

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kesho Januari 26 watacheza kwenye uwanja ambao wanaweza kucheza kutokana na ubora wa uwanja huo.

Pablo amekuwa kwenye mwendo mgumu na kikosi cha Simba ndani ya dakika 180 katika viwanja vya ugenini ambapo hajaambulia ushindi zaidi ya sare na safu yake ya ushambuliaji haijafunga bao.

Ilikuwa ni kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Sokoine na ubao ulisoma Mbeya City 1-0 Simba na ule wa pili ilikuwa ni Mtibwa Sugar 0-0 Simba Uwanja wa Manungu.

Kesho Januari 26 Simba itakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar ambao nao pia wanahitaji pointi tatu kwenye mchezo huo.

Pablo amesema:”Kesho tunacheza mchezo wetu wa ligi kwenye mchezo ambao tunaamini kwamba tunacheza kwenye uwanja ambao tunaweza kucheza tupo tayari kwa ajili ya kusaka ushindi.

“Utakuwa mchezo mgumu hilo tunalijua lakini tupo tayari kuhusu mechi zetu ambazo zimepita ni sehemu ya mchezo hivyo kesho tutacheza na wachezaji wapo tayari,” amesema.

Simba imekusanya pointi 25 kibindoni baada ya kucheza mechi 12 inakutana na Kagera Sugar iliyo nafasi ya 11 na imekusanya pointi 13 baada ya kucheza mechi 12.

Kikosi kimefanya leo mazoezi ya mwisho na miongoni mwa nyota ambao wamefanya mazoezi ni pamoja na Hencok Inonga, Mohamed Hussen, Bernard Morrison na Clatous Chama.

Previous articleABDI BANDA NYOTA WA MTIBWA SUGAR AOMBA RADHI
Next articleMASTAA NIGERIA WATISHIWA MAISHA