Home International MASTAA NIGERIA WATISHIWA MAISHA

MASTAA NIGERIA WATISHIWA MAISHA

WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Nigeria, Maduka Okoye ambaye ni golikipa na kiungo Alex Iwobi inaelezwa kuwa wametishiwa kuuwawa baada ya timu yao ya taifa kuondolewa kwenye mashindano na Tunisia siku ya Jumapili.

Kutokana na vitisho hivyo golikipa wa timu ya taifa ya Nigeria, Okoye alifunga sehemu ya wafuasi wake kuweza kuacha ujumbe kwenye machapisho yake (comment), huku Iwobi ambaye alitolewa dakika ya 66 kwa kupewa kadi nyekundu naye alipokea vitisho vya kuuwawa, sababu ni timu yao kufungwa kwenye michuano hiyo ya AFCON 2021.

Iwobi baada ya kupata vitisho hivyo naye aliiweka akaunti yake “archived” kwa muda ili asiweze kuona vitisho ambavyo Wanaigeria walikuwa wanamtishia na kuonekana kuwa wao ndio sababu ya timu hiyo kutofuzu hatua ya 16 bora.

Mashabiki wengi wa Nigeria baada ya mchezo kuisha walitumia mitandao ya kijamii kuelezea hisia zao za kutoridhishwa na matokeo ambayo timu ya taifa  waliweza kuvuna kwenye michuano ya AFCON 2021, pia baadhi ya wachezaji walitumia mitandao ya kijamii kuweza kuwasihi mashabiki wasiwatishe baadhi ya wachezaji kupitia mitandao.

Previous articlePABLO:TUTACHEZA KWENYE UWANJA AMBAO TUNAWEZA KUCHEZA
Next articleKISA KUVULIWA UBINGWA,MWAKINYO ASEMA NI WIVU TU