Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, ameripotiwa kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuinoa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Azam FC imefanikiwa kumbakisha kocha huyo licha ya kuwepo kwa tetesi kwamba alikuwa tayari amefikia makubaliano ya awali na Chama cha Soka cha Mali kwa ajili ya kuifundisha timu ya taifa ya nchi hiyo.
Ibenge, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amekubali kuendelea kubaki Dar es Salaam baada ya mazungumzo ya kuboresha masharti ya mkataba kufanikisha makubaliano kati yake na uongozi wa klabu.
Hatua hiyo inazima tetesi za kuondoka kwake, huku Azam FC ikiendelea na msimu ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 52.