Afrika Yaandika Historia Kombe la Dunia la FIFA 2026, Yapeleka Timu 10

Afrika imeweka rekodi mpya ya kihistoria baada ya kupata wawakilishi 10 katika Kombe la Dunia la FIFA 2026, litakalofanyika Marekani, Canada na Mexico kuanzia Juni 11, 2026.

Nchi zilizofuzu ni pamoja na Senegal, Morocco, Misri, Ghana, Algeria, Tunisia, Ivory Coast, Cape Verde, Kongo (DRC)  na Afrika Kusini.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya soka Afrika kuwa na timu 10 kwenye fainali za Kombe la Dunia, hatua inayoonesha ukuaji mkubwa wa kiwango cha soka barani humo.

Kuongezeka kwa nafasi za Afrika kunatokana na FIFA kupanua mashindano hayo kutoka timu 32 hadi 48, jambo lililotoa fursa zaidi kwa mataifa yanayoendelea kisoka.

Morocco bado inaendelea kubaki mfano baada ya kufanya vizuri hadi hatua ya nusu fainali mwaka 2022, huku mataifa kama Cape Verde yakipata nafasi ya kwanza kushiriki mashindano hayo makubwa.

Kwa ujumla, hatua hiyo inatajwa kuwa mwanzo wa enzi mpya ya soka la Afrika katika jukwaa la dunia.