Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, imekosa ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana wa umri huo (AFCON U-17) baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 4-2 dhidi ya Senegal katika mchezo wa fainali uliopigwa usiku wa kuamkia leo.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya mabao 1-1 ndani ya dakika 90 za kawaida kabla ya Senegal kuibuka mabingwa kupitia changamoto ya mikwaju ya penalti. 
Tanzania ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Mihambo dakika ya 7 ya kipindi cha kwanza na kuwapa matumaini mashabiki wa Serengeti Boys.
Hata hivyo, Senegal walirejea mchezoni dakika ya 64 kupitia bao la Dione na kufanya mchezo huo kwenda kwenye mikwaju ya penalti baada ya sare kuendelea hadi mwisho wa mchezo.
Katika penalti, Senegal walionyesha utulivu mkubwa baada ya kufunga mikwaju yote minne waliopiga huku Tanzania wakifunga penalti mbili na kukosa mbili.
Kwa ushindi huo, Senegal U-17 wametwaa ubingwa wa AFCON U-17 kwa mara ya pili katika historia yao baada ya kufanya hivyo pia mwaka 2023.
Matokeo:
Senegal πΈπ³ 1-1 πΉπΏ Tanzania
(Penalti: 4-2)
Wafungaji:
β½ 07β Mihambo (Tanzania)
β½ 64β Dione (Senegal)
Penalti:
πΈπ³ β
β
β
β
πΉπΏ β
β
ββ
