Home Sports KISA KUVULIWA UBINGWA,MWAKINYO ASEMA NI WIVU TU

KISA KUVULIWA UBINGWA,MWAKINYO ASEMA NI WIVU TU

BAADA ya Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBF), kuwavua mikanda yao ya ubingwa wa Intercontinetal, Hassan Mwakinyo na Ibrahim Class, hatimaye bondia Hassan Mwakinyo ameibuka na kuvunja ukimya kwa kusema kuwa yeye na uongozi wake haujui chochote zaidi ya kudai kuonewa wivu.


Mwakinyo ametoa kauli hiyo 
kufuatia WBF kuwavua mkanda ya ubingwa huo, kwa kuzingatia kanuni inayotamka kuwa bondia akishindwa kutetea ubingwa wake ndani ya miezi sita tangu aupate, basi atavuliwa.

Rais wa shirikisho hilo, Howard Goldberg, raia wa Afrika Kusini, amethibitisha kuvuliwa ubingwa kwa mabondia hao.


Mwakinyo ametumia 
mtandao wa kijamii wa Instagram kujibu tuhuma hizo kwa kusema kuwa watu wanatakiwa wapuuzie suala la yeye kuvuliwa ubingwa huo kwa kuwa hajui kitu chochote kama mhusika kutokana na kutokupewa taarifa yoyote huku akienda mbali akiamini ni suala la yeye kuonewa wivu na baadhi ya vyombo vikubwa vya habari nchini.

“Puuzeni hizo stori za kuvuliwa mkanda, mimi mhusika na timu yangu hatuna hizo taarifa, watu wasipate uthubutu wa kudanganya umma bila wahusika wa timu kuhakiki na kama ni kweli,”.

Previous articleMASTAA NIGERIA WATISHIWA MAISHA
Next articleLEO, UWANJA WA KAITABA NI KAGERA SUGAR V SIMBA