Home Sports ABDI BANDA NYOTA WA MTIBWA SUGAR AOMBA RADHI

ABDI BANDA NYOTA WA MTIBWA SUGAR AOMBA RADHI

BEKI wa Mtibwa Sugar, Abdi Banda amewaomba radhi wadau wa soka nchini Tanzania kufuatia kauli aliyoitoa dhidi ya wachezaji wa Simba.

Banda alitoa kauli ya kuwakejeli kwa wachezaji wa Simba, baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Manungu Complex Jumamosi Januari 22 na timu hizo kwenda sare ya 0-0.

Beki huyo ambaye amewahi kucheza soka Afrika Kusini kabla ya kurejea nchini msimu huu 2021/22, ameomba radhi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

“Tuanze wiki mpya yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Huenda niliwaudhi au kuwakera wengi kila mmoja kwa nafasi yake naomba mnisamehe sana.

“Kwenye mpira au kwenye mchezo wowote kuna maneno ya kejeli na dharau kwa mpinzani wako au hata mchezaji mwenzako lakini haimaanishi kuna uhasama kama wengi walivyopokea maneno yangu. Michezo ni furaha na ajira basi tusichukulie kila kitu personal/serious sana.

“Naomba mnisamehe sana maana kila mtu ana upokeaji wake na tafsiri yake. Sikuwa na lengo la kumbagua Henock Inonga au wachezaji wengine wa Simba SC. Tusahau yaliyopita, tupo kwa ajili ya kujenga na kuutangaza mpira wetu na sio chuki wala ubaguzi wowote hasa kwa wachezaji wanaokuja kucheza hapa kwetu,” amesema Banda.

Katika mchezo huo Banda alifanya kazi yake kwa umakini akiwa pamoja na mshikaji wake Ibrahim Ame ambaye yupo hapo kwa mkopo akitokea Simba.

Previous articleNYOTA MPYA YANGA AMPA JEURI MTUNISSIA
Next articlePABLO:TUTACHEZA KWENYE UWANJA AMBAO TUNAWEZA KUCHEZA