Home Sports NYOTA MPYA YANGA AMPA JEURI MTUNISSIA

NYOTA MPYA YANGA AMPA JEURI MTUNISSIA

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ujio wa kiungo mshambuliaji,Mkongomani, Chico Ushindi, umeongeza ubora na ushindani wa namba katika kikosi chake.

Nabi amesema kuwa licha ya kuwa na nafasi ya kumtumia Fei Toto, lakini yupo Chico ambaye anamudu kucheza nafasi hiyo namba kumi.

Nabi amesema kuwa anaamini uwezo mkubwa alionao Chico kutokana na kumfahamu baada ya kumfuatilia tangu akiwa klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.

Aliongeza kuwa Chico ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja namba 7, 10 na 11 hivyo uwepo wake katika timu, unampa nafasi kubwa ya kuwepo katika kikosi chake cha kwanza.

“Chico ana faida kubwa katika timu, hiyo ni kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja katika timu, hivyo ninaamini atatoa mchango mkubwa katika timu.

“Hivyo ushindani utaongezeka katika timu baada ya Chico kuja, hivi sasa kilichobakia kwake ni kuingia
katika mfumo ambacho ni kitu kidogo, hilo ni jukumu langu ambalo nitalifanya,” amesema Nabi.

Yanga ni vinara kwenye ligi wakiwa na pointi 35 baada ya kucheza mechi 13 inafuatiwa na Simba iliyo nafasi ya pili na pointi 25 baada ya kucheza mechi 12.

 

Previous articleBREAKING: MASHABIKI WA SIMBA WAPATA AJALI KAHAMA, SITA WAJERUHIWA
Next articleABDI BANDA NYOTA WA MTIBWA SUGAR AOMBA RADHI