DAKIKA 90 zimekamilika kwa wababe wawili kumtambua mshindi nani katika mchezo wa NBC Premier League uliokuwa na ushindani mkubwa.
Mwisho ubao wa Uwanja wa Amaan Zanzibar umesoma Yanga SC 3-0 Azam FC, pointi 3 zikibaki kwa wenyeji wa mchezo Juni 24, 2026 ikiwa ni mzunguko wa pili.
Magoli yamefungwa na Ibrahim Bacca dakika 41, Depu dakika ya 73 kwa mkwaju wa penati na Pacome dakika ya 81 zikiwa zimesalia dakika 8 mpira kugota mwisho.
Matokeo haya yanaifanya Yanga SC kuongoza msimamo ikiwa na pointi 69 baada ya mechi 28 imebakiza mechi mbili kukamilisha mzunguko wa pili.
Katika mchezo wa mznguko wa kwanza wababe hawa walitoshana nguvu kwa kushuhudia ubao ukisoma Azam FC 0-0 Yanga SC.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.