Mtibwa Sugar 0-3 Simba SC

UBAO wa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro umesoma Mtibwa Sugar 0-3 Simba SC ikiwa ni NBC Premier League mzunguko wa pili kwa wababe hawa wawili.

Mabao yamefungwa na Rushine dakika ya 9 kwa penati, Seleman Mwalimu dakika ya 77 na Anicent Oura dakika 90.

Matokeo haya yanaifanya Simba SC kufikisha pointi 67 nafasi ya pili tofauti ya pointi 2 na vinara wa ligi Yanga SC wenye pointi 69 wote wamecheza mechi 28.

Walipokutana mzunguko wa kwanza wababe hawa wawili waligawana pointi mojamoja, hivyo mchezo wa mzunguko wa pili umeamua mbabe wa kuvuna pointi 3 muhimu.

Katika msako wa pointi 6, Simba SC imevuna pointi 4 mbele ya Mtibwa Sugar inayotumia Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kwa mechi za nyumbani.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.