UONGOZI wa Simba SC umebainisha kuwa umeanza mpango wa kuhesabu siku kuelekea tamasha kubwa la Simba Day ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa 2026/27.
Mwenyekiti wa Bodi, Crescentius Magori amesema : “Hii maana yake tumeanza count down kuelekea kwenye Simba Day. Kama kuna mkoa Simba tukija huwa tunasikia raha ni Arusha kuna wakati mwingine huwa nafatilia kwa mkuu wa mkoa kuuliza ule uwanja unaisha lini. Nadhani mkoa ambao utakuwa wa kwanza kupata shughuli ya Simba Day kwa miaka ijayo ni Arusha sababu ya ule uwanja.
“Simba ilikuwa ya kwanza kusupport utalii kwa Visit Tanzania, lakini kama mnakumbuka mwaka juzi tulizindua jezi kwa kibegi na kikaenda Mlima Kilimanjaro. Mwaka huu tumeamua kusherekea miaka 90 na kusherekea Wiki ya Simba kupitia hifadhi ya Ngorongoro. Niwahakikishie kwa kushirikiana na Simba itakuwa na faida kwa taasisi zote mbili.
“Niwahakikishie mmefanya maamuzi sahihi kushirikiana na Simba. Simba inawafuasi kwenye mitandao zaidi ya milioni 20, kwahiyo ushirikiano huu ambao tutafanya na countdown hadi tunakwenda kuzindua tutapata wateja wengi sana wa ndani na nje. Tutumie wakati huu kutangaza product nyingi kwelikweli. Sisi tunakuhakikishia tutakusupport, tupo tayari kusupport hifadhi, utalii na uchumi wa nchi hii uzidi kupaa.”