Home International NYOTA MAN UNITED AIBUKIA SEVILLA

NYOTA MAN UNITED AIBUKIA SEVILLA

KLABU ya Sevilla ya Hispania imefikia makubaliano ya kumsajili kwa mkopo winga wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Antony Martial.

Nyota huyo amekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha United na amekuwa akishinikiza kuondoka ndani ya miamba hiyo.

Sevilla wamekubali kulipa mshahara wote wa mchezaji huyo hadi mwezi Juni na atasafiri leo kuelekea Hispania kukamilisha taratibu za kujiunga na miamba hiyo iliyowahi kuja Tanzania  kumenyana na Simba kwenye mchezo wa kirafiki.

Previous articleKOCHA WA MAKIPA YANGA AFUNGUKA DIARRA KUKAA BENCHI AFCON
Next articleAZAM WATANGAZA ABDI KUWA KOCHA MKUU