TIMU ya taifa ya Burkina Faso imekuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya robo fainali ya AFCON kwa kuiondosha timu ya taifa ya Gabon kwa changamoto ya mikwaju ya penati 7-6 Baada ya timu hizo kumaliza dakika 120 kwa sare ya kufungana 1-1.
Gabon licha ya kucheza pungufu kwa muda mwingi wa mchezo huo,wameonesha ushindani mkubwa na kutoa tafsiri nyingine ya ugumu wa michuano hiyo inayoendelea huko Cameroon.
Zilipigwa jumla ya penati 9, Gabon wamekosa 3 na Burkina Faso wakakosa 2. Burkina Faso katika robo fainali watakutana na Tunisia iliyoshinda mbele ya Nigeria kwa bao 1-0.
Tayari waliokuwa wanautetea ubingwa huo wamefungashiwa virago walikuwa ni Algeria ambao wamemaliza michuano hii mapema kutokana na kupewa asilimia kubwa kushinda kwa mara nyingine mwisho wa siku wameangukia pua.