Home Sports CHIKO USHINDI AMPA KIBURI NABI, USHINDANI WA NAMBA NI BALAA!

CHIKO USHINDI AMPA KIBURI NABI, USHINDANI WA NAMBA NI BALAA!

KOCHA Mkuu wa Yanga, raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, amesema kuwa ujio wa kiungo mshambuliaji,
Mkongomani, Chico Ushindi,
umeongeza ubora na ushindani wa namba katika kikosi chake.


Kauli hiyo aliitoa siku moja
kabla ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania uliotarajiwa kupigwa jana saa
kumi kamili kwenye Uwanja
wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.


Kabla ya mchezo huo, kocha
huyo alitangaza kuwepo hatihati ya kumtumia kiungo wake mshambuliaji
Feisal Salum ‘Fei Toto’
kutokana na majeraha.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Nabi alisema kuwa licha ya kuwepo hatihati ya kumtumia Fei Toto, lakini yupo Chico ambaye anamudu kucheza nafasi hiyo namba kumi.


Nabi alisema kuwa
anaamini uwezo mkubwa alionao Chico kutokana na kumfahamu baada ya kumfuatilia tangu akiwa klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.


Aliongeza kuwa Chico
ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja namba 7, 10 na 11 hivyo uwepo wake katika timu, unampa nafasi kubwa ya kuwepo katika kikosi chake cha kwanza.


“Chico ana faida
kubwa katika timu, hiyo ni kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja katika timu, hivyo ninaamini atatoa mchango mkubwa katika timu.


“Ka
tika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania, huenda tukamkosa Fei Toto kutokana na majeraha, lakini tayari yupo Chico mwenye uwezo wa kucheza na fasi yake.


“Hivyo ushindani
utaongezeka katika timu baada ya Chico kuja, hivi sasa kilichobakia kwake ni kuingia
katika mfumo
ambacho ni kitu kidogo, hilo ni jukumu langu ambalo nitalifanya,” alisema Nabi.

Previous articleSABABU YA MUKOKO KUSEPA YANGA HII HAPA
Next articleKOCHA WA MAKIPA YANGA AFUNGUKA DIARRA KUKAA BENCHI AFCON