
NANI KUVUNJA REKODI YA MAYELE YANGA?
USIKU wa deni haukawii kukucha, ndivyo unavyoweza kusema kwani hatimaye kivumbi cha mashindano ya kimataifa yaani Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika kimeanza kutimua vumbi rasmi Ijumaa na kinatarajiwa kuendelea wikiendi hii. Kwa upande wa Tanzania Bara msimu huu tunatarajiwa kushirikisha timu nne katika mashindano hayo, ambapo timu za Yanga na Simba…