Home Sports KIMATAIFA KAZI BADO HAIJAGOTA MWISHO

KIMATAIFA KAZI BADO HAIJAGOTA MWISHO

TUMEONA namna ambavyo wawakilishi wetu kwenye anga la kimataifa wakiendelea kupambania kombe kufikia malengo ambayo yapo na kila mmoja akiwa anahitaji kuona ushindi unapatikana.

Kila timu inaona namna ambavyo kazi inafanyika kutokana na msako wa ushindi kwenye mchezo husika. Ipo hivyo mashindano ya kimataifa hayana mwenyewe ila atakayefanya maandalizi mazuri ni njia nyepesi kupata matokeo.

Malengo ya msimu uliopita ni muhimu kuyatazama na kujua ni wapi yalipoishia kisha kuanza upya pale ambapo yalikwama kwenda sawa ili kuendelea kuwa imara zaidi kwa msimu mwingine katika anga la kimataifa.

Hakuna muda wa kuanza kulaumiana kwa sasa zaidi ni kufanyia kazi makosa ili kuendelea kusonga mbele kwa ajili ya wakati ujao ambao utakuwa bora zaidi.

Muda hausubiri kwenye anga la kitaifa na kimataifa vitu vinakwenda kasi na hakuna suala la kusubiri kitakachotokea bali ni lazima kujipanga kwa ajili ya kupata kile ambacho kinatakiwa kwenye kila idara.

Wale ambao walishindwa kutumia nafasi kwenye mechi za mwanzo basi wakipata nafasi wakati ujao ni muhimu kuonyesha uwezo wao kwa kufanya kweli kwa mara nyingine tena.

Mwanzo wa ligi tunaona ushindani umekuwa mkubwa hivyo ni muhimu uendelee mpaka mwisho wa ligi hapo tuna amini ututazidi kuwa bora. Mwendelezo huo uwepo na kimataifa kwa wale ambao walipata matokeo chanya.

Kimataifa wameanza kuona picha itakavyokuwa kwenye mechi zijazo na zile ambazo walicheza hii ina maana kuwa kila kona ushindani ni mkubwa na kupata ushindi inawezeka.

Iwe nyumbani ama ugenini kitu cha msingi ni kupambana kwa umakini na kupata matokeo mazuri hilo litaongeza nguvu ya kujiamini na kupata matokeo mazuri kwenye mechi zinazofuata.

Kwa kuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wawakilishi wa Tanzania walianza ugenini basi nyumbani kazi iwe kubwa zaidi a ile ambayo ilifanyika ugenini. Kwenye Kombe la Shirikisho Singida Fountain Gate kete yao ilianza nyumbani hivyo kazi ugenii iwe moja kusaka ushindi.

Kila kitu ili kiwe bora na chenye kuvutia kwenye maisha ya soka kinahitaji maandalizi mazuri hivyo tu basi inawezekana na tunaamini kila kitu kitakuwa sawa.

Muhimu kila mmoja kuhakikisha anatimiza wajibu wake kwa umakini na muda uliopo ni sasa hakuna ambaye anapenda kupata matokeo mabaya.

Pia ni muhimu wachezaji kuongeza nidhamu wawapo eneo la mafunzo na wakiwa nje ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza viwango vyao.

Nidhamu ni kitu cha muhimu katika kutimiza majukumu yote na inaongeza uelewa hata pale ambapo mchezaji anakuwa hajaelewa inakuwa rahisi kwa benchi la ufundi kumpa mbinu nyingine zaidi.

Mashabiki wanapenda kuona matokeo mazuri kwenye mechi zote hivyo wachezaji ni muhimu kuendelea kulitambua hilo na kulifanyia kazi.

Tunatambua kwamba mnajua kuhusu jambo la dakika 90 kuwa na ushindani mkubwa lakini ni muhimu kuendelea kuwa kwenye ubora kila wakati ukizingatia matokeo mazuri ni furaha kwa Watanzania wote.

Mbali na mechi za kimataifa ikumbukwe kwamba ligi bado inaendelea kwa kuwa yale mapumziko yamegota mwisho hivyo kazi bado ipo palepale.

Previous articleAFYA YA WACHEZAJI NI MUHIMU, WACHEZAJI LINDANENI
Next articleGAMONDI AJA NA MPANGO KAZI WA KUVURUGAVURUGA