SIMBA NA YANGA KIMATAIFA, NCHI IPO KAZINI

    MAPIGO ya moyo kwenda kasi katika kiwango chake hiyo ni afya, ikitokea kukawa kuna jambo la tofauti limetokea kwa wengi tutasema nchi ipo kazini.

    Mastaa wa Yanga na Simba leo wana kazi kubwa kusaka ushindi kwenye anga la kimataifa ambapo Watanzania watakuwa wanasubira kuona kitakachovunwa baada ya dakika 90.

    Ni leo Jumamosi saa 10 jioni, Uwanja wa Kigali Pele nchini Rwanda Al Merrik watavaana na Yanga. Simba wao kibarua chao itakuwa ni Uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia.

    Hapa tunakuletea majeshi ya timu hizo zinazoipeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la kimataifa namna hii:-

    Ulinzi kamili

    Bakari Nondo Mwamnyeto nahodha wa Yanga hatakuwa kwenye kikosi cha leo kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi kitakachowakabili Al Merrikh kutokana na sababu za kifamilia.

    Yeye ni beki ila mikoba yake itakuwa kwa mabeki wengine wa kazi ambao ni pamoja na Dickson Job, Ibrahim Bacca na Gift Fredy ambao hawa wana uwezo wa kutimiza majukumu yao uwanjani.

    Mbali na nyota hao pia Kibwana Shomari, Lomalisa Mutambala, Nickson Kibabage na Yao Kouassi hawa ni walinzi ndani ya Yanga.

    Kwa upade wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ni Shomari Kapombe, David Kameta, Israel Mwenda, Mohamed Hussein, Henock Inonga, Che Malone na Kennedy Juma hawa watakuwa kwenye upande wa ulinzi kimataifa.

    Mikono salama

    Aishi Manula kipa namba wa Simba hatakuwa langoni kwa kuwa anaendelea kupata matibabu. Mikoba yake ipo kwenye mikono ya Ally Salim.

    Mbali na uwepo wa Salim pia yupo Hussein Abel na Ayoub Lakred. Kwa Yanga kuna mdaka mishale Djigui Diarra, Metacha Mnata na Aboutwalib Mshery hawa ni kwa upande wa makipa.

    Ushambuliaji

    Kwenye eneo la ushambuliaji Gamondi ana vijana wake wa kazi  kwenye majukumu yao kimataifa.

    Maxi Nzengeli mwenye jezi namba saba mgongoni hana mambo mengi ni pasi ndefu na spidi kwake ni msingi, Pacome Zouzoua, Clemet Mzize mzawa, Kennedy Musonda na Hafiz Konkoni.

    Kwa upande wa Simba wanaye Jean Baleke, Moses Phiri, John Bocco na Shaban Chilunda.

    Watengeneza mipango

    Kiungo Aziz KI yupo Rwanda akijiunga na timu hiyo moja kwa moja kwa kuwa alikuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Burkina Faso. Kazi ya mapigo huru ipo kwenye mguu wake wa kushoto.

    Mbali na Aziz KI yupo Jesus Moloko, Dennis Nkane, Farid Mussa, Skudu Makudubela ambaye alikuwa nje kwa muda akipambania hali yake akiwa anaanza kurejea kwenye ubora wake.

    Ni Clatous Chama mwamba wa Lusaka, Willy Onana,Saido Ntibanzokiza wapinzani wao Power Dynamo wanamtambua kwenye mchezo wa kirafiki alionyesha njia ya kutoa pasi zote mbili za mabao yupo pia Luis Miquissone.

    Watibua mipango

    Jonas Mkude, Zawadi Mauya, Mudhathir Yahya, Khalid Aucho, Salum Aboubhakari. Ni wataalamu kwenye kuvuruga mipango ya wapinzani huku wakiwarahisishia kazi washambuliaji kucheka na nyavu kwa upande wa Yanga.

    Ndani ya Simba kuna Mzamiru Yassin kiungo punda, Sadio Kanoute mzee wa kutembeza mabuti kimyakimya, Kibu Dennis mtu wa kazikazi.

     

    Previous articleYANGA YATEMBEZA MKWARA HUU KIMATAIFA
    Next articleKIMATAIFA: POWER DYNAMO 1-0 SIMBA