Home Sports YANGA YATEMBEZA MKWARA HUU KIMATAIFA

YANGA YATEMBEZA MKWARA HUU KIMATAIFA

KUELEKEA mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merreikh Waarabu wa Sudan, uongozi wa Yanga umeweka wazi kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya kupata ushindi katika mchezo huo.

Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi inatarajiwa kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merreikh unaotarajiwa kuchezwa Septemba 16.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Rwanda ikiwa ni hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya makundi.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa malengo makubwa ni kufanya vizuri katika mashindano yote na kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wanahitaji kupata matokeo ikiwa ni pamoja na mechi yao dhidi ya Al Merreikh.

“Mechi zetu zote ni muhimu ambacho tunahitaji ni matokeo mazuri tuna amini kila kitu kitakwenda sawa hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi katika mechi zetu zote.

“Katika ligi ya mabingwa Afrika malengo yetu tunahitaji kufika katika hatua ya makundi, ili tupate hiyo nafasi ni muhimu kuanza kufanya vizuri kwenye mechi hizi za mwanzo,” amesema Kamwe.

Miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao wapo Rwanda ni pamoja na Zawadi Mauya, Gift Fred, Jesus Moloko, Aziz KI.

Ikumbukwe kwamba mara ya mwisho Yanga kutinga hatua ya makundi ilikuwa ni 1998.

Previous articleHUYU HAPA SIMBA KUMTUMIA KIMATAIFA
Next articleSIMBA NA YANGA KIMATAIFA, NCHI IPO KAZINI