HUYU HAPA SIMBA KUMTUMIA KIMATAIFA

BAADA ya kushuhudia kikosi chake
kikipangwa kuvaana na Al-Ahly katika
mchezo wa robo fainali ya Kombe la African
Football League, kocha mkuu wa Simba
Mbrazil, Robert Olivieira ‘Robertinho’
amefunguka uwepo wa Luis Miquissone
ambaye amewahi kuichezea Al Ahly ni faida kubwa kwao katika kupata baadhi ya mbinu
za kuwamaliza.

Simba leo ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamo na watani zao wa jadi Yanga watakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Al Merreikh ya Sudan..

Kwenye upande wa African Football League kupitia droo ya mashindano
hayo ambayo ilifanyika Makao Makuu ya
Shirikisho la Soka Afrika (Caf) jijini Cairo
Misri, Simba walipangwa kuvaana na Al Ahly
katika hatua ya robo fainali ya mashindano
hayo ambayo itakuwa na michezo miwili
Oktoba 20, na 24, mwaka huu.

Luis, ambaye amejiunga na Simba kupitia
dirisha hili kubwa la usajili ametokea ndani
ya kikosi cha Al-Ahly aliyoichezea kwa
kipindi cha misimu miwili kabla ya kufikia
makubaliano ya kuvunja mkataba na
mabosi hao wa zamani na kurejea Simba
kutokana na kukosa nafasi ya kucheza akiwa
na mabingwa hao wa Afrika.

Robertinho amesema: “Kwa sasa mawazo
yetu yote yapo katika kuhakikisha
tunashinda mchezo wetu wa kwanza wa
mtoano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya
Power Dynamos ya Zambia.

“Lakini tumeifuatilia droo ya Jumamosi na
tunajua tunakwenda kukutana na Al Ahly
ambao ni mabingwa wa Afrika na miongoni
mwa timu bora na ngumu barani Afrika,
lakini tunaamini kwenye  ubora wa kikosi
tulichonacho na tuna faida ya kuwa na Luis
ambaye anajua taarifa nyingi za wapinzani