KOCHA YANGA AFICHUA SIRI HII YA 5G

KOCHA Mkuu wa Yanga Muargentina
Miguel Gamondi amezipa tahadhari timu za
Ligi Kuu Bara. Hiyo ni baada ya timu yake
kuanza vema kwa kushinda mechi mbili
mfululizo mabao 5-0 walipocheza dhidi ya
KMC na JKT Tanzania.

Yanga pia ilipata ushindi wa mabao 5-1
walipocheza dhidi ya ASAS FC ya nchini
Djibouti katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Gamondi amesema kuwa  timu pinzani
hazitakiwi kujilinda zaidi wanapokutana na
badala yake kufunguka kwa kucheza soka
kama hawataki kufungwa tano.

Kocha huyo wa Yanga leo ana kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Merrikh ya Sudan.

Gamondi amesema wapinzani wakiwa wanacheza kwa kujilnda wanawapa ruhusa ya kufanya mashambulizi kwa kasi huku wakianza
kuwakabia kuanzia golini kwa wapinzani.

“Wapinzani wenyewe ndio wanataka
tuwafunge mabao matano, ni kutokana na
kucheza soka la kujilinda kwa kukaa wengi
golini kwao.

“Wao kama hawazitaki tano, basi wasijilinde
na badala yake wanapaswa kushambulia
kwa kucheza soka la pasi. Kwani wakijilinda sisi tunapata nafasi ya kushambulia goli la wapinzani kwa kasi tukiwatumia viungo kupiga pasi za mabao,”  amesema Gamondi.