SHABIKI wa Klabu ya Yanga Paulo Martin ameshinda Sh120,989,610 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet.
Martin ni mjasiriamali alikabidhiwa fedha zake na Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi katika hafla fupi iliyofanyika hivi karibuni Dar.
Mushi alisema kuwa Martin anaungana na washindi wengine mbalimbali ambao wameshinda mamilioni kupitia droo ya Perfect 12 na kuweza kubadilisha maisha yao.
“Martin anakuwa mmoja wa wanachama wa nyumba yao ya mabingwa ambao kwa sasa imesheheni mamilionea mbalimbali. Tunaposema M-Bet ni nyumba ya mabingwa tunakuwa na maana maalum, mpaka sasa tumewazadia mamilioni washindi mbalimbali” alisema Mushi.
Alisema kuwa M-Bet itaendelea kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia michezo yake mbalimbali ya kubashiri na kuwaomba watu wenye umri kuanzia miaka 18 kushiriki.
“Kubashiri si kazi, naomba watu wajue, ni burudani ambayo inakufanya kuibuka milionea endapo utashinda.M-Bet inajisikia fahari sana kuendelea kuwatoa washindi na kubadili maisha yao,” alisisitiza Mushi.
Kwa upande wake, Martin alisema kuwa alianza kubashiri miaka mitatu iliyopita na anashukuru ndoto zake kutimia.
“Nimeanza kubashiri kupitia M-Bet na sijahama kwa sababu ni kampuni imekuwa ikitangaza washindi wengi. Nimeona washindi wengi na nikaamini kuwa ipo siku na mimi nitakuwa natangazwa kwa ushindi. Ndoto yangu imetimia. Nitatumia fedha hizo kwa kuendelea biashara zangu na shughuli nyingine za kimaendeleo,” amesema Paulo.