Mechi 6 za Namungo FC 2026/27, wanaanza na Yanga SC

 Namungo FC wana mechi 6 kali ambazo ni dakika 540 za mwanzo ndani ya NBC Premier League na watafungua pazia kwa kusaka pointi 3 muhimu dhidi ya Yanga SC, Uwanja wa Majaliwa, Agosti 15.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda ilimaliza msimu wa 2025/26 ikiwa nafasi ya 10 ilikusanya pointi 34 baada ya kucheza mechi 30 itakutana na timu iliyomaliza na pointi 75 mchezo wa kwanza.

Mchezo wa pili utapigwa Agosti 18 itakuwa dhidi ya Geita Gold na kete ya 3 wakiwa nyumbani Uwanja wa Majaliwa itakuwa dhidi ya Fountain Gate ya Ofisa Habari Issa Mbuzi ambaye ametamba kuwa wapo tayari kwa msimu mpya wa 2026/27.

Agosti 25 itakuwa ni mchezo wa kwanza ugenini watakaribishwa na JKT Tanzania, wazee wa mapigo na mwendo itapigwa Uwanja wa Jenerali Isamuhyo na Septemba Mosi watakuwa kwenye kibarua dhidi ya Singida Black Stars, Uwanja wa Airtel.

Mchezo wa 6 utakaokamilisha dakika 540 za mwanzo watakuwa ugenini ni Septemba 11 kukabiliana na Dodoma Jiji, utapigwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.