Yanga imekataa ofa ya USD 700,000 (takribani TSh bilioni 1.8) kutoka FAR Rabat kwa ajili ya kumsajili kiungo mshambuliaji Allan Okello.
FAR Rabat walituma ofa hiyo jana, lakini Yanga imeikataa na kuwaeleza kuwa Okello ataondoka endapo klabu hiyo itakuwa tayari kulipa USD milioni 1.5 (takribani TSh bilioni 3.9).
Yanga inaamini Okello ana thamani kubwa sokoni, ikimlinganisha na aliyekuwa nyota wao Feisal Salum “Fei Toto”.
Wakati huo huo, Wydad AC pia imeanza kufuatilia uwezekano wa kumpata Okello.
Soko la Okello limeanza kuwa moto!