Petro de Luanda 🇦🇴 imetangaza rasmi kumsajili tena mshambuliaji wa Kimataifa wa Angola, Laurindo Dilson Maria Aurélio ‘Depú’, kutoka Young Africans SC 🇹🇿, kuelekea msimu wa 2026/27.
Uhamisho huo umegharimu USD 500,000, sawa na takribani TSh bilioni 1.3. 💰
Kupitia taarifa yao, Petro de Luanda wamemkaribisha Depú kwa kusema:
“Ameirejea katika sehemu ambayo anakuwa mwenye furaha. Karibu tena, Depú!” 💛💙❤️🎉