MABOSI wa Simba SC wanatajwa kufikiria kuanza mazungumzo na muuaji wa Yanga SC,Tonny Talasi aliyefunga mabao 2 katika Wiki ya Mwananchi, Uwanja wa Uhuru.
Simba SC imepishana na mshambuliaji iliyekuwa naye msimu wa 2025/26, Seleman Mwalimu ambaye ametambulishwa kwa watani zao wa jadi Yanga SC tayari kwa changamoto mpya msimu wa 2026/27.
Taarifa zinaeleza kuwa mara baada ya mchezo wa Yanga SC 1-2 Les Aigles du Congo uongozi wa Simba SC ulianza kumfuatilia mchezaji huyu mwenye miaka 20.
Rais wa Heshima wa Simba SC hivi karibuni aliweka kuwa wapo tayari kwa usajili na pesa ipo bank ikihitajika itatumika.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.