RASMI Agosti 11,2026 Seleman Mwalimu ametambulishwa ndani ya kikosi cha Yanga SC akitokea kikosi cha Wydad Casablanca kwa mkopo.
Ikumbukwe kwamba mchezaji huyu msimu wa 2025/26 alikuwa ndani ya kikosi cha Simba SC ambapo alifunga jumla mabao 9 katika NBC Premier League.
Mwalimu anakumbukwa kuwa miongoni mwa wachezaji aliyefunga goli la ushindi kwenye mchezo wa fainali ya Muungano ilikuwa dhidi ya Yanga SC.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Yanga SC imeeleza namna hii: “Seleman Gomez ni Mwananchi tuliwaambia anafanya mazoezi na timu ndogo, anakuja kuanza msimu na klabu kubwa,”.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.