Leo ni burudani tupu! Mataifa makubwa yashuka dimbani

Je unajua leo hii ni siku ya burudani ndani ya dakika 90 za mwamuzi?. Mataifa makubwa Dunia kushuka dimbani kusaka furaha yako leo. Burudika na mechi hizi sasa.

UEFA Nations League kule Ulaya bado inarindima ambapo leo hii  Uingereza atakuwa kibaruani dhidi ya Czechia mchezo ambao upo Kundi A, huku vijana wa Thomas Tuchel wakiwa wanaingia uwanjani wakiwa na morali kubwa baada ya kushinda kwa kishindo mechi iliyopita.

Safu ya ushambuliaji imekuwa na makali, huku Harry Kane, Bukayo Saka, Anthony Gordon na Jude Bellingham wakiwa na uwezo wa kutengeneza nafasi na mabao na hiyo inampa upana zaidi kocha wa timu hiyo kubadilisha wachezaji muda wowote.

Huku Czechia wao wametoka mepoteza dhidi ya Hispania 3-1 na pia Uingereza iliifunga 2-0 kwenye mchezo wao uliopita, hivyo itahitaji kuwa na nidhamu kubwa hasa kwenye ulinzi. The Lions wanaonekana kuwa na kasi na ubunifu zaidi, lakini Czechia inaweza kusumbua ikiwa itacheza kwa kujilinda kwa mpangilio na kutumia mashambulizi ya kushtukiza.

Bila kusahau kuwa mechi hizi zote unaweza kuzipata pale Meridianbet ambao pia wanakupa taarifa kuhusua misimamo ya makundi haya ya UEFA Nations League na yale ya AFCON.

Kivumbi kingine kitakuwa kwenye mechi ya Croatia dhidi ya Hispania ambao ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi mnono leo.

Croatia anaingia kwenye mchezo huu akiwa na presha kubwa ya kupata matokeo baada ya kupoteza mchezo uliopita kwa mabao 7-0 dhidi ya Uingereza, huku nyuma yake pia akipoteza kwa mabao 4-1 dhidi ya hapo Hispania.

Croatia inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na presha kubwa baada ya kupigwa 7-0 na Uingereza, huku siku chache kabla pia ikifungwa 4-1 na Hispania.

Wakati vijana wa Luis de la Fuente kwa upande mwingine wako kwenye kiwango kizuri sana, huku wakiwa wameshinda mechi zao tano za mwisho na tayari wameifunga Croatia kwenye mchezo wa kwanza. Lamine Yamal ndiye mmoja wa silaha kubwa, huku mfumo wao wa kumiliki mpira na kuharakisha mashambulizi ukiwa changamoto kwa Croatia.

Kwa Croatia wachezaji tengemezi ni kama vile, Luka Modrić, Mateo Kovačić na Andrej Kramarić ambao wanahitaji kurejesha utulivu na ushindani wa kiungo, huku safu ya ulinzi ikiwa lazima iwe makini zaidi dhidi ya kasi ya Yamal na wachezaji wa pembeni wa Hispania. Je nani kushinda leo?.

Huku Afrika michuano ya kufuzu AFCON 2027 kuendelea kwa mchezo mmoja leo ambapo Angola atamenyana dhidi ya Malawi huku tofauti yao mpaka sasa ikiwa ni pointi 2 pekee kwenye msimamo wa Kundi B.

Angola inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na pointi moja baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Misri, huku ikiwa haijapoteza katika mechi saba kati ya nane zilizopita. Kwa upande mwingine, Malawi ilianza kampeni ya kufuzu AFCON 2027 kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Sudan Kusini, hivyo itakuwa na morali nzuri.

Hata hivyo, mchezo huu unatarajiwa kuwa wa ushindani na wenye kushambuliana kwa zamu kwani pointi 3 zinahitajika na kila timu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwenye michuano hii.

Malawi imekuwa na changamoto katika ufungaji, huku Angola nayo ikiwa na rekodi ya sare nyingi hivi karibuni. Historia ya mechi hizi pia inaipa Malawi matumaini, kwani imepoteza mchezo mmoja tu kati ya nane zilizopita dhidi ya Angola.

Ingia pale Meridianbet na ujue ni wachezaji gani ambao watakuwepo na ambao ni majeruhi, lakini pia unaweza ukajua ni nani anayeongoza kwa magoli mengi mpaka sasa.